Monday, May 31, 2010

MY BABY IS YOUR BABY


Kwa kweli inatia huruma sana pale mtoto mdogo anapofikwa na majanga mazito,rakini mimi mtazamo wangu ni mtoto wangu ni mtoto wako

CAMERA YANGU (JICHO LA TATU)






Ali Choki aliingia na staili ya aina yake ndani ya ukumbi wa Msasani Club jana usiku tayari kwa utambulisho wa Bendi yake ya Extra Bongo. Baadae staili hiyo ilikuja kujulikana kama Igwee...! Choki haishi Vituko, Ni Burudaanii...tu.

WAKUSWAMPA KITAA



MZEE PWAGU AZIKWA


Mzee Pwagu, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 88, kwenye Hospitali ya Amana, Ilala majira ya saa 10 alasiri na kuzikiwa siku iliyofuata kwenye makaburi ya Kigogo CCM, Dar.
Ijumaa Wikienda lilikuwepo wakati wa mazishi na kushuhudia umma wa watu waliojitokeza kwa wingi kumsindikiza mzee Pwagu kwenye safari ya dawamu.

Wasanii wengi walifika kwenye mazishi hayo ambapo walieleza kusikitishwa kwao.
Walisema kuwa mzee Pwagu alikuwa mlezi wa wasanii wengi hasa wa maigizo na kwamba muongozo wake umesaidia kuwaweka kwenye ramani.
Katibu wa Kundi la Kaole Sanaa, Simon Simalenga ‘Mr. Dimera’ alisema kuwa Pwagu ni mwenyekiti muasisi wa kundi hilo ambalo lilianzishwa mwaka 1998.

“Alishirikiana na watu sita, akiwemo Mama Haambiliki, Cristant Mhenga, Chuma Suleiman ‘Bi. Hindu’, Fatuma Rajabu ‘Bi. Kidide’ na Said Fundi ‘Mzee Kipara,” alisema Mr. Dimera.
Kwetu sisi, Pwagu alikuwa shujaa kwa sababu jitihada zake, uvumilivu na kujitolea ndivyo vimewezesha sanaa ya maigizo kukubalika Tanzania, kukua na kuzaa soko la filamu.

Iliandikwa kwamba lazima watu wengine watengeneze barabara halafu wengine wapite, Mzee Pwagu atabaki kukumbukwa kwa ujenzi wake wa sanaa ambao unawezesha ajira ya vijana wengi hivi sasa.
Mungu ni sababu ya kila kitu.
Inna Lillah Wainna Ilayh Rrajiuun.

Saturday, May 29, 2010

MCHARAZO WA Bi MKUBWA


HAMEKUONA AMEKUPENDA,Je nikweli amekupenda?
Bi mkubwa,Huyo mtu amekutamani na wala ajakupenda,unajua sisi binadamu hatujui kutofautisha kati ya kupenda na kutamani?ninachotaka kukuelezeeni watu kama nyie hukiona mtu wa namna hii muepukie mbali,watu kama hawa huwa hawakosi jiji.
UMFANYIE NINI MPENZI WAKO HUKIWA UNAMAUMBILE MADOGO?
Bi mkubwa,Ongeza mahaba ya kuzikamata hisia zake(kumuandaa)kabla ya tendo la ndoa.
KUGEUZA URAFIKI KUWA MAPENZI.
Bi mkubwa,Zipo gia mbili za kumwingilia rafiki yako ili awe mpenzi, lakini kubwa zaidi hapa ni kwamba ili kumteka kirahisi, ni vizuri ukaongeza ukaribu, hivyo kuwa naye pamoja kwa muda mwingi na katika sehemu mbalimbali.
Kufanya hivyo, itakusaidia uzidi kumteka na kukuona wewe ni sawa na ubavu wake. Muda ambao atakuwa mbali na wewe, atajiona kama kapungukiwa na kitu fulani mwilini ambacho ni uwepo wako. Taswira ikawa ya namna hiyo, ujue kuwa hata ukimwingizia yale mambo yetu(ushirikina) hawezi kupindua,tahadhari yangu kwako ni mapenzi ya ushirikina uwa haya dumu.
TUONANE WIKI IJAYO

WAKUSWAMPA KITAA





VIJIMAMBO DUNIANI





Friday, May 28, 2010

BREAKING NEWS


Habari iliyotufikia sasa hivi aliyekuwa msanii wa kaole Mzee Pwagu amefariki dunia nusu saa iliyopita katika hospital ya Amana jijini Dar es salaam.Habari kamili kuhusu msiba huo wa Marehemu Mzee Pwagu tutawaleteeni katika blog yenu kujua maziko na wapi msiba utakuwa.Mungu amuweke mahali pema pepon Amen

CAMERA YANGU (JICHO LA TATU)












Monday, May 10, 2010

MC CHICHI AFARIKI


Mc Chichi alikuwa maarufu sana hapa Dar es salaam kwa kuiendesha na kusherehesha shughuli hasa kitchen party na send off.