Saturday, March 26, 2011

KIBARAZAN KWE2







Asha Baraka mkurugenzi wa twanga asets alikuwa ni mwenyekiti wa chama ambacho kimeundwa na wao wenyewe kwa ajili ya kuweza kuchangia misaada ya pesa kwa ajili ya kuweza kuzipatia familia za marehemu wa 5 stars.Kupitia leo tena tuliweza kusaidiana kukusanya rambirambi ambazo jana zilichukuliwa na kupelekwa huko kwa wahusika.

Tunawashukuru Mbunge wa kinondoni Idd Azzani,Umoja wa wanawake wa CCM(UWT),Baraza la sanaa la Taifa.Pia band mbalimbali za muziki nchini Twanga pepeta,Fm Academia,Akudo Impact na The Kilimanjaro band wana njenje.
Pia watu mbalimbali ambao walikuwa wakichangia kwa njia ya MPESA kutoka mikoani kote Tanzania na wananchi ambao walienda kuchangia kwa kule Temeke.Wengine walifika kule kinondoni makao makuu ya Twanga pale Aset pasipo kusahau clouds fm radio pia ilitoa rambirambi zao.
Hayo ndiyo yaliyojili kibarazan kwe2 wiki hii.

ADHABU MBELE YA KANISA





Baadhi ya wakazi wa Kizuiani Mbagala wakiuangalia maiti ya mmoja wa watuhumiwa wa wizi, aliyeuawa na wananchi wenye hasira mbele ya Kanisa la Anglikana leo alfajiri baada ya kufanya jaribio la wizi lililoshindikana

WAKUSWAMPA KITAA












Tutawakumbuka siku zote na miaka yo ni pengo zito kwa namna moja hama jingine itachukua muda sana kulisahau ila MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI AMIN.Ni bdhi ya maombolezo mazito ambapo ni msiba uliotokea siku ya tarehe 21/3/2011 wakiwa wanatokea katika zira zao za mikoani walianza Ifakara,Makambako,Na kumalizia Kyela wakati wanarudi wakapatwa na umauti huo Baada dereva wa basi walilopanda kulivaa roli la mbao na hatimae kupinduka na kupoteza maisha ya wasanii hao.Kiukweli inauma na inasikitisha kuona baadhi ya waimbaji na wapiga vinanda tegemeo la bendi hiyo wote wameaga dunia kilichobaki kuwaombea ndugu zetu wapumzike salama AMIN

Saturday, March 19, 2011

WAKUSWAMPA KITAA






Leo jumamosi saa 4 Asubuhi mtaani kwetu kulitokea tukio la kustusha kilichowafanya wakazi wa mtaa wetu hasa maeneo ya jirani waje kujionea.tukio lenyewe ni la huyo mtoto hapo juu anayenyweshwa maziwa,mtoto huyo aliingia chumba cha mpangaji wa mama yake na kuzama uvunguni na kutoa chupa ambayo ndani yake ilikuwa na dawa ya madoa na kuanza kuinywa dawa hiyo,mama wa mtoto huyo alimuona mwanaye hakitapika na kuishiwa nguvu kwa dakika kadhaa ndipo alipoinusa chupa aliyoishikilia mtoto wake na kubaini ilikuwa na dawa ya madoa ambayo ilisibitishwa na mpangaji wa chumba hicho kwa jina la habiba,mpaka naondoka eneo la tukio mtoto huyo anaendelea vizuri huku mama yake hakijiandaa kumpeleka mtoto wake hospital.Wakuswampa kitaa

Thursday, March 17, 2011

HARAKATI ZA KUSAKA HABARI



Nikiwa mitaani huwa bize na kazi,hapa kiwa kitaani maeneo ya magomeni kagera,huku kitaa ndiko kunakotupatia habari za wakuswampa kitaa.

LOLIONDO





Loliondo hapatoshi kama utakuwa mfatiliaji mzuri wa vyombo vya habari hili si jambo geni kwako .Loliondo kwa Mchungaji mstaafu Ambilike Ambwakise kwa kupata dawa ya mitishamba na kupona pia dawa hiyo huambatana na maombi kwa imani yako utapona . watu wengi wamejitokeza na kukimbilia kwa baba ukweli foleni haifai na tiba inatolewa kwa kiasi kidogo cha pesa shilingi 500 tu.


WAKUSWAMPA KITAA
















Hayo ndiyo yaliyotokea siku ya jumapili ndani ya ufukwe wa coco beach.