Wednesday, April 27, 2011

CHEZEA MANCHESTER UNITED WEWE?







Wapenzi na mashabiki wa timu yetu tuipendayo ya Man U tunajipongeza kwa ushindi tulioupata jana.

KIPENGERE KINGINE KINAKUJA

Hukurasa au Mada nyingine itakayokuwa inausu NYETI KULIKO NYETI ULIZO NAZO ndiyo kinakuja wiki ijayo na msimamizi wake mkuwa ni mjomba Mo wa ukweli
NYETI KULIKO NYETI ULIZO NAZO

MASHINE YA KISASA ZAIDI



Hizi mashine wazungu wanaingizwa humu ndani kisha mtu anafunikwa, Anapikwa mpaka apate ile rangi flani ambayo anaipenda yeye,Binadamu huwa tunatamani kile tusichokuwa nacho, wakati wa Afrika wanajikoboa kuwa weupe wadhungu nao wanataka rangi ya Chocolate

SIJUI NIKIPI KITAKACHO TOKEA BAADAYE


MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.

Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.

Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.

Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.

Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe.

Saturday, April 23, 2011

WAKUSWAMPA KITAA





Hali hii ilitokea leo mchana mitaa ya home kwetu magomeni kagera jiji dar es salaam.

Wednesday, April 20, 2011

40 YA 5 STARS




Machozi, simanzi na huzuni vimeibuka upya wakati wa kuhitimisha siku 40 za msiba wa vifo vya wanamuziki 13 wa Kundi la Five Stars Modern Taarab waliopoteza maisha kwa ajali ya gari huko Mikumi, Morogoro usiku wa Jumatatu ya Machi 21, mwaka huu.

Tukio hilo la hitma lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita ambapo lilihudhuriwa na kadamnasi kutoka sehemu mbalimbali, nje na ndani ya jiji.
baadhi ya wanamuziki walionusurika kwenye ajali hiyo wakitokwa na machozi hivyo kuibua upya vilio kwa mastaa na watu wengine waliokuwa wakiwakumbuka marehemu kifamilia na kimuziki.


“Unajua watu wakikumbuka ajali yenyewe ilivyokuwa, lazima watokwe machozi,” alisema mmoja wa wakurugenzi wa kundi hilo, Ferouz Juma na kuongeza:
“Kwa sasa ni vigumu kufikiria kurudi upya kwa kundi letu kwani wengi wetu tuna vitu vinatusumbua vichwani.

“Bado wanamuziki wetu walionusurika wanahitaji muda wa ziada kulitafakari lile tukio.
“Kila mmoja akimtazama mwenzake hapa anatokwa na machozi hasa wakivuta hisia kwa wenzao waliopoteza maisha wakiwa wanawaona.”

ZENA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Mwimbaji mkongwe wa kundi hilo aliyedumu katika muziki wa mwambao kwa zaidi ya miaka kumi, Zena Mohamed ambaye alinusurika kifo kwenye ajali hiyo alilieleza gazeti hili kuwa, amepoteza imani na muziki hivyo hafikirii kurejea tena jukwaani.
Alitoa kilio chake kuwa, tangu lilipotokea tukio hilo na yeye kuponea chupuchupu, amekuwa akisumbuliwa na ndoto za ajabu ajabu kila kukicha.
Alifunguka: “(Huku akitokwa machozi) Nahisi kama Israel mtoa roho za watu ananifuata kila ninapokwenda.
“Achilia mbali kupanda jukwaani ambako sitaki kusikia, lakini hata nikiwa nyumbani hali ya maruweruwe huwa inanijia mara kwa mara kichwani

MAREHEMU
Katika ajali hiyo waliopoteza maisha ni pamoja na Issa Ally ‘Kijoti’, Husna Mapande, Sheba Juma ‘Jasusi’, Omary Hashim na Hamisa Mussa.
Wengine ni Ramadhan Maheza ‘Kinyoya’, Omary Tall, Samir Maulid, Hajji Mdahaniwa, Hassan Ngereza, Maimuna Makuka ‘Kisosi’, Hajji Babu na Tizo Mgunda.

NI KWELI MVUA INALETA HAMASA YA NGONO?




Kwa sasa mvua ina nyesha...kuna mtu kanifata ananiambia mpenzi wake ana mwambia awahi kutoka ofisini leo kwani ana hamu nae na hiki kimvua ndo usipime.Akaniuliza hivi mvua huwa inaleta hamu ya kufanya ngono?mie sikuwa najibu kwa sababu mie binafsi huwa napenda kulala wakati mvua inanyesha nje.Nikasema nikuulize mdau ni kweli haya mambo mvua huleta hamu na kama ni kweli kwa nini??
KWANGU MIMI
1.mvua haihamasishi ngono ila ni baridi ambalo linatokana na mvua ndoo liufanya mwili kuchemka na kuwa na uhitaji,so wanawake wengi wawe makini kwenye kipindi kama hichi coz mimba ziko nje nje 2nashindwa niseme nn hapa ila kama ingekuwa baridi inaleta hamasa basi nchi za wenzetu zenye baridi na mvua kwa mda mrefu ingekuwa balaa kwa kuzaana. kwangu binafsi naona niuamuzi wa mtu na mtu mana hata kama mvua inanyesha kama hujaandaa mazingira ya kungonoka basi huwezi kufanya hicho kitendo. Du wadau kungonoka kunahitaji kuandaliwe banaaaaaaa.3 Si kweli ni fikra na hisia za watu kuwawazia wapenzi wao kuwa kwa sababu mvua hairusu mtu kutoka nje au kuwa mahali fulani zaidi ya ndani ya nyumba basi watu huwaza saa hizi ningekuwa nimejifungia na fulani.

Mmmhh Waswahili kwa kudata na ngono hawajambo 4Hapa nawaachia wadau mchakachue

MZIGO SOKONI




Kutoka kushoto ni JACKLINE PENTZEL, WEMA SEPETU pamoja na ROSE NDAUKA kwa pamoja wanaunda kundi linaloitwa JAROWE ambapo wana malengo mengi sana kwenye Industry ya Filamu BONGO.. kwasasa hivi wamekuja na filamu yao mpya kabisa inayoitwa THE DIARY kama cover yake inavyoonekana hapo juu.. UNAIONAJE COVER...!!???
Huu ni muonekano wa Cover ya PART TWO... THE DIARY coming soon kutoka JAROWE ambapo ni kifupi cha JACKY,WEMA na ROSE

Tabasamu! Ahaaa Unachekaaa?










NAJUA WAJUA.LAKIN UJUI UNACHOJUA.


Hii ni Hotel ya JULES UNDERSEA LODGE iliyojengwa chini ya Bahari huko Florida nchini MAREKANI. Ujenzi wake ilikamilika mnamo mwaka 1986 na imejengwa umbali wa mita 6.4 kuelekea chini ya Bahari. Sasa basi kupanga masaa 3 tu ndani ya Hotel hiyo inakulazimu ulipie Dola 250 ambazo ni sawa na 380,000 za kibongo, na ukitaka kulala kwa usiku mmoja utalipia Dola 380 sawa na 560,000 za kibongo, HABARI NDIO HIYO...

HADITHI YA UKWELI KUTOKA LOLIONDO


Hii ni hadithi ya ndugu yangu mmoja aliyekwenda LOLIONDO majuzi. Anasimulia hivi, ni usiku wenye baridi kali, mvua inayoambatana na upepo inanyesha. Katika hali ya kawaida, baridi hii haivumiliki kwani nawaona kina baba wakiota moto katika jiko linalotumiwa na mama lishe.Natamani kuungana nao lakini nashindwa kwani jiko lenyewe ni dogo na idadi ya watu waliolizunguka ni kubwa. Lakini pia ugeni wangu katika eneo hilo unakuwa kikwazo cha shauku yangu ya kujiunga nao.Mbele yangu nawaona kina mama na watoto wao wengi kiasi, wakiwa wamelala barazani katika moja ya nyumba za wageni zilizopo katika eneo liitwalo Wasso.Wasso ni kitongoji maarufu katika eneo la Loliondo. Kitongoji hiki ni sehemu ya mji wa Loliondo na kwa mujibu wa wenyeji wa mji huu, Wasso ni mji mpya unaopanua ukubwa wa mji wa asili wa Loliondo.Eneo hili linachangamshwa na uwepo wa shughuli nyingi za kibiashara, nyumba za wageni na hata gulio kubwa ambalo hufanyika kila Jumamosi likiwavuta wafanyabiashara wengi kutoka nchini Kenya. Lakini usiku, halitamaniki kutokana na baridi kali.Katika baraza au kwenye veranda ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayi, ndipo walipolala kina mama hawa. Udadisi wangu unabaini kuwa hawa ni wenyeji wa maeneo ya Wilaya ya Ngorongoro na wako safarini kwenda Samunge kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila kunywa dawa.“Usiku umewakuta hapa hivyo lazima walale halafu kesho asubuhi na mapema, wanaamka kwenda kwa babu kunywa dawa," anasema mmoja wa wahudumu wa nyumba ya wageni aliyejitambulisha kwa jina moja la Fatma na kuongeza: “Hapa ni kawaida, tena leo wamepungua, huwa wanakuwa wengi hadi tunawatimua (kuwafukuza). ”Nilimwuliza Fatma kwamba watu hawa wanatumia usafiri gani kwenda Samunge? Jibu lake lilikuwa ni fupi tu kwamba “…..hawa wanatembea”. Umbali kutoka Wasso hadi Samunge ni karibu kilometa 70 lakini, kwa mujibu wa wenyeji, matumizi ya njia za mkato huwawezesha kupunguza umbali huo hadi kufikia kilometa zisizopungua 40.Kwa maana hiyo wenyeji wanasema hutumia muda wa kati ya saa tano hadi sita kufika Samunge na baada ya kupata kikombe cha babu huanza tena safari ya kutembea kurudi makwao. Ng’ambo ya barabara kutoka ilipo nyumba hii ya wageni ya Sayi, ipo nyumba nyingine ya kulala wageni iitwayo Selemani. Hivyo jibu la Fatma lilinipa wajibu wa kuvuka barabara ili kwenda kuona iwapo kuna watu wengine waliolala barazani.Hali niliyoikuta ni ileile. Kina mama kwa kina baba walikuwa wakihangaika kujisitiri kwa mashuka na makoti waliyokuwa nayo. Katika hali ya ubinadamu, nawahurumia lakini sina la kufanya kwani hata kama ningekuwa na fedha za kugharamia malazi yao, vyumba katika nyumba za wageni zilizopo Wasso zilikuwa zimejaa. Malazi kwa Babu Samunge Wakati fulani nikiwa Loliondo, nililazimika kulala katika Kijiji cha Samunge ambako Mchungaji Mwasapila anatoa dawa ya magonjwa sugu.Siku ya kwanza tulipoamua kwamba tutalala Samunge mimi na wenzangu, Mussa Juma na Fidelis Felix tuliazimia kutafuta sehemu ya kulala usiku ule. Wakati tukiwa katika harakati za kutafuta malazi, nilibaini kwamba watu wengi ambao wanasubiri zamu za kunywa dawa hawana mahali pa kulala. Wengi wamechukua mikeka mabusati na kuyatandika pembezoni mwa magari yao na kulala hapo. Wengine wamekuwa katika foleni, wakilala kwa ‘staili’ hii kwa muda wa siku sita au zaidi.Lakini hawa wana ahueni kwani wana uwezo wa kufanya hivyo. Kuna wengine ambao maisha yao ni magumu zaidi ya haya. Hawa wanalala kwenye magari hasa magari makubwa kama malori mengine yakiwa ni Fuso. Humo kuna watu ambao wako taabani. Hawa hawalioni jua kwani hawana uwezo wa kutoka nje. Kutwa, kucha wamo ndani ya magari yao wakisogea taratibu kuelekea kwa Mchungaji Mwasapila.Katika gari mojawapo aina ya Fuso lililokuwa likitokea mkoani Mara, kulikuwa na abiria wasiopungua 100, wakiwemo wazee, watoto na wagonjwa ambao walikuwa hawajiwezi. Lakini pamoja na adha hiyo, watu wote katika eneo hilo wanavumilia tabu hizo wakiwa na shauku kubwa ya kukutana na Mchungaji Mwasapila ili awape kikombe. Kambi za mahemaKatika kutafuta malazi, tuliingia katika eneo lenye mahema na kuanza kuulizia gharama za kukodi kwa usiku mmoja.Katika eneo la kwanza tulionyeshwa mahema ya aina tatu. Moja ni hema ambalo kulala kwa usiku mmoja gharama yake ilikuwa Sh60,000. Hema hili ni kubwa na lina magodoro mawili madogo ya shule (futi mbili na nusu kwa tano).Pia tukapelekwa kwenye hema lenye ukubwa wa kati ambalo lilikuwa na godoro moja dogo. Gharama yake ni Sh45,000.Hema la tatu lilikuwa dogo na gharama yake ni Sh35,000. Hema hilo lilikuwa na godoro moja ndani. Kwa kuangalia uwezo wetu kifedha, tulilazimika kutafuta eneo jingine na baada ya kuzunguka katika maeneo kadhaa, tulibahatika kupata hema kwa gharama ‘nafuu’ ya Sh25,000. Hema hilo kwa mujibu wa msimamizi wake, lilikuwa na uwezo wa kulaza watu watatu kwa wakati mmoja. Katika eneo lile kulikuwa na mahema yasiyopungua 20 na wakati tulipofika, saa 4.20 usiku, lilikuwa limebaki hema moja tu, ambalo ndilo tulilopewa na kulipa kiasi hicho cha fedha. Hema hili liligeuka kuwa makazi yetu ya muda kwani kila tulipofika kulala Samunge katika siku zote 14 tulizokaa Loliondo, tukiendelea na kazi zetu za kihabari, tulikuwa tukilitumia. Usiku wa taabuUsiku wa kwanza ulikuwa wa tabu kwetu kutokana na hema hilo kuwa na dogoro moja tu dogo. Ilibidi tuweke vichwa na sehemu ya viwiliwili vyetu kwenye godoro hili huku sehemu ya miili yetu ikibaki chini katika ‘sakafu’ ya hema hilo ambalo kwa jinsi lilivyotengenzwa ni kama suti kuanzia sakafu, kuta mpaka paa. Hatukuwa na shuka, blanketi, kanga wala kitenge kwa ajili yakujisitiri na baridi. Pamoja na kwamba Samunge si sehemu yenye baridi ya kutisha, lakini ulipofika usiku wa manane, tulilazimika kuyatafuta majaketi na makoti yetu.Baridi ilianza kuingia katika miili yetu kwa mbali. Kweli, ulikuwa ni usiku wa tabu na kila mmoja wetu alitamani kuche haraka ili tuweze kuondokana na adha hiyo. Haya yalithibitika asubuhi pale kila mmoja wetu alipokuwa akiusimulia ‘usiku wake’ ulivyokuwa. Ulifika wakati tukataka kuweka azimio la kutolala tena Samunge lakini, kwa jinsi mazingira yalivyokuwa, azimio hili halikutekelezeka kwani tulirejea kulala kijijini hapa mara tatu zaidi.Hali hii inanikumbusha usiku wa mvua na baridi kule Wasso ambako kina mama na watoto wao walikuwa wamelala barazani baada ya kukosa malazi. Nilijiuliza moyoni, ikiwa sisi ambao tumepata hema tunapata tabu kiasi hicho, hali ilikuwaje kwa wale waliolala nje bila hata ya kuwa na nguo ya kujisitiri?Pamoja na hali hii, watu bado walionekana kuwa na shauku kubwa ya kufika Samunge kupata kikombe kwa Mchungaji Mwasapila.Mwisho

UNAWAKUMBUKA? MAIGIZO YAO JE?






Hao ni baadhi ya watu ambao ambao waliwahi kushika sana kupitia vipindi vya kwenye LUNINGA(tamthilia) na kwa enzi hizo walikuwa juu sana kupitia michezo yao.. mimi nawakumbuka.. vipi wewe unawakumbuka!!??? kama ndio Unaweza kunitajia majina yao kuanzia huyo wa kwanza mpaka wa mwisho na nini kilikuwa kinakufurahisha kwa kila mmoja...
UNAWAKUMBUKA HAO!!!???

JICHO LA 3 (MY CAMERA)