Saturday, September 21, 2013

TRUE

NYETI KULIKO NYETI HULIZO NAZO

MAPOZI

Wewe unaic yup mkali zaid ya mwenzie?

KWETU

lady jay dee

Chorus: Yahaya unaishi wapi Kwani jina lako halisi nani Yahaya eeehh Oooh Yahaya, Oooh Yahaya, Oooh Yahaya Maskani yako Kinondoni Nyumba namba haijulikani Yahaya eeeehh Oooh Yahaya, Oooh Yahaya VERSE 1: Huyu kijana mwenzetu, Kila siku tupo nae maskani Anakula ofa za watu, Anapoishi hata hapajulikani Tumetafuta, tumeuliza, hakuna ajuae Anavyozuga, anavyopita Si umdhaniae Na hafananii kabisa, na fix anazofanya Akidanganya kwa kina Unaingia kingi unafuata, kumbe hana helaaaa Longo longo nyingi Rudia Chorus: VERSE 2 Kwa story za vilingeni, Utafikiri kweli yeye ndio boss Suruali zake na mashati, Anasema anafanya kazi bank Mara anasema usalama wa Taifa, Hakuna ajuae Kalubandika wa kizazi kipya, usomdhaniae Na hafanii kabisa, na fix anazofanya Akidanganya kwa kina Unaingia kingi unafuata, kumbe hana helaaaa Ooooh Yahaya Rudia Chorus: Mara anasema usalama wa Taifa Hakuna ajuae Kalubandika wa kizazi kipya Uso mdhaniae Na hafanii kabisa na fix anazo fanya Akidanganya kwa kina, unaingia kingi unafuata Kumbe hana helaa Chorus: Yahaya unaishi wapi Kwani jina lako halisi nani Yahaya eeehh Oooh Yahaya, Oooh Yahaya, Oooh Yahaya Maskani yako Kinondoni Nyumba namba haijulikani Yahaya eeeehh Oooh Yahaya, Oooh Yahaya MWISHO: Mtunzi/ Mwandishi: Judith Wambura ( Lady JayDee) Producer: Man Water Studio: Combination Sound

WAKUSWAMPA KITAA

WANAWAKE wawili walioolewa katika familia moja ‘wajengez’, mama Hashimu na mama Fadhila, wakazi wa Kimara King’ong’o jijini Dar, hivi karibuni walifikishwa serikali za mtaa kwa kosa la kutukanana matusi ya nguoni pamoja na kushikana uchawi, mcharazo linakunyetishia. Inadaiwa kuwa wanawake hao ‘walimwagiana’ matusi hayo usiku wa manane na kusababisha watu wengine kukosa usingizi na kukusanyika kuwasikiliza. Mara baada ya kufikishwa serikali ya mtaa, wake wenza hao walitakiwa kueleza ugomvi wao na kila mmoja kuanza kushusha tuhuma kwa mwenzake. Mapaparazi wetu waliwashuhudia wakati wake wenza hao walipokuwa wakijieleza mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ong’o, Demetrius Mapesi na Mtendaji wake Amina Rashid. Mama Hashimu alianza kuelezea kisa kizima na kufuatiwa na mama Fadhila (pichani) ambaye wakati akijieleza alipandisha mori kiasi cha kumfanya atake kumrukia mwenzake. “Unajua nasikia hasira sana kwa sababu mama Fadhila ameniita mchawi huko mtaani unadhani mimi nitaelewekaje? Ukweli kauli hiyo inaniuma sana,” alisema mama Hashim na kuangua kilio. Hata hivyo, baada ya kila mmoja kueleza ya moyoni, mwenyekiti wa serikali za mtaa pamoja na mtendaji wake, waliwaamuru wake wenza hao kupeana mkono na kuombana msamaha. “Sasa hapa hakuna kesi, kwani wote mna makosa, hebu niambieni mnawafundisha nini watoto wetu kwa matusi mliyotukanana hadharani?” alihoji mwenyekiti na kuwataka wayamalize mambo hayo. Aidha, mwenyekiti huyo aliahidi kuwafuatilia ili kuona kama watakuwa wamebadili tabia zao. Kama vile haitoshi aliwaahidi kama watarudia atawahamisha mtaa pamoja na waume zao kwani mtaani kwao hawahitaji watu wanaotukanana ovyo na kuzushiana mambo ya kichawi. Baada ya tamko la mwenyekiti, mtendaji wake aliwaamuru wake wenza hao kuandika matusi waliyotukanana kisha akawapiga faini ya shilingi 20,000 kila mmoja. “Kutokana na matusi yenu nalazimika kuwapiga faini ya shilingi elfu ishirini kila mmoja, ingawaje kwa mujibu wa sheria ya Tanzania mtu akikutwa na hatia ya kutukana anatakiwa kutozwa faini ya shilingi elfu hamsini au kufungwa jela miezi sita,” alisema mtendaji huyo. Kila mmoja alilipa nusu ya faini na kuahidi kumalizia huku wakisema kuwa hawatarudia kufanya kosa hilo tena