Tuesday, November 2, 2010

KEVIN HATUA BONGO


Mshindi wa Big brother revolution mwaka jana KEVIN CHUWANG akiwa na familia yake ametua hapa bongo kwa ajili ya kutoa mahali ya dada yetu Elizabeth tayari kwa maandalizi ya harusi yao itakayofanyika mwezi wa pili mwakani.Katika moja ya vikao vyake hapa Dar Kevin aliniita ili kushauriana mambo kadha wa kadha juu ya harusi yao lakini pia juu ya project zake anazotarajia kufanya Africa mashariki.Binafsi nilianza kujuana na Kevin katika jumba la big brother revolution mwaka jana ambapo mimi nilikuwa humo kama star mwalikwa tu,wakati naondoka katika jumba hilo baadhi ya housemate kama Hannington,Leonel nk waliniomba nguo zangu lakini Kevin yeye aliomba nimpatie jina la The great,nami nilimwita Kevin The great nikimwambia kuwa atakuwa the great wa jumba hilo,hatimae alishinda na kuzidi kuwasiliana nami.

No comments:

Post a Comment