Tuesday, October 12, 2010

KIBARAZANI KWETU





Mwanamuziki mahiri nchini katika miondoko ya Taarab, Jokha Kassim ‘Queen of Golden Voice’, amekamilisha vibao vyake vinne vipya vinavyokamilisha albam itakayokuwa na jumla ya nyimbo nne huku akiwashirikisha wanamuziki mahiri katika miondoko hiyo, walionaksh na kunogesha vilivyo albam hiyo,Albam hiyo itakayobebwa na kibao cha ‘Wacha Nijishebeduwe Mke Mwenzangu Unijue’ kilichotungwa na mtunzi mahiri wa mashahiri ya miondoko hiyo, Amin Salmin Abdul.

Mtunzi wa kibao hicho kinachotarajia kuteka hisia za mashabiki wa miondoko hiyo, Amin, alisema kuwa katika albam hiyo pia kutakuwa na vibao kama, Kelele za mlango, uliotungwa na Salum Vuai na kuimbwa na Jokha Kassin, ambao pia muziki umeandaliwa na kwa ushirikiano wake mwenyewe Jokha Kassim na Thabit Abdul.

Alizitaja nyimbo nyingine zinazokamilisha albam hiyo kuwa ni pamoja na MSG za Nini, ambao shairi lake limeandaliwa nae Amin Salmin Amour na kuimbwa na Jokha Kassim na muziki kunakshiwa nae Thabit Abdul ‘Mtoto wa Ilala’, pamoja na Kinyang’anyiro hukiwezi, ambao pia umeimbwa na Jokha Kassim, uliotungwa na Amin Salmin Amour na muziki kuandaliwa na Thabiti Abdul.

Aidha Amin, alisema kuwa Uzinduzi wa albam hiyo unatarajia kufanyika Novemba 21 katika Ukumbi wa Travertine Magomeni Jijini Dar es Salaam, ambapo pia kutakuwa na shoo za utangulizi kutoka kwa waimbaji mahiri wa miondoko hiyo, Khadija Koppa na Isha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ na kusindikizwa na kundi zima la Jahazi Morden Taarab

No comments:

Post a Comment