Tuesday, October 12, 2010

WAKUSWAMPA KITAA





Dada mmoja mkazi wa mburahati kwa jongo amepatwa na maswaiba ya ajabu na historia ktk maisha yake,Ni mjamzito hapo alipo ila hali ndio hiyo akiwa mahali hata kama ni kwako akikaa peke yake moto unawaka aidha kwenye nguo zake,kochi,kitanda,hata kama ni nguo iliyotundikwa inawaka moto.Mpaka sasa haijaeleweka ni kwa nini mashekhe wamemuombea dua toka juzi hiyohiyo ambapo alilala msikitini.

Wapo waliosema labda kachukua mume wa mtu kafanyiwa mchezo lakini alipoulizwa akasema huyo mwanaume mwenye mimba wamefunga ndoa na anavyojua kamkuta hana mwanamke labda awe kamdanganya.

Dada wa watu hana raha kabisa ndugu zake inabidi wakae nae kama kumetokea msiba maana ni kitu cha ajabu sana kilichompata ndugu yao maana kimeanza wiki hii hapa.

No comments:

Post a Comment