Sunday, August 29, 2010

KIBARAZANI KWETU KUNA NINI?



Mshiriki wa mwaka jana wa Big Brother Revolution kutoka Tanzania Elizabeth Gupta jumamosi iliyopita ya tarehe 21 nchini Nigeria alivalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake ambae ndie mshindi wa Big Brother revolution ya mwaka jana Kevin Chuwang Pam kutoka Nigeria.
Wapenzi hao ambao walikuwa katika ukumbi wa Ogus Baba Laugh Goes On ambako hufanyika onyesho la comedy walipanda pamoja on stage kuperfom wimbo kwa pamoja unaoitwa 'unapata mambo'....mmh kumbe bidada nae huwa anaimba!!.Walipomaliza kuimba Kevin akapiga magoti kwa Elizabeth na kumwambia “Elizabeth, will you marry me”.
Ukumbini kulikuwa na watu takribani 2000 ambao walikuwa wakipiga kelele “say yes, say yes, say yes” ...Elizabeth akasema "Yes"
Hongera kwenu tunasubiri ndoa walianza kama utani tu,nakumbuka wakiwa ndani ya jumbaKevin alikuwa akisema anampenda sana Eliza.Kweli kwenye maisha ya mapenzi huwezi kujua utaishia kuwa na nani nakumbuka Eliza alikuwa anasema hajawahi kuwa na wapenzi/wanaume weusi hasa wa kiafrika!!!!

No comments:

Post a Comment