Saturday, March 20, 2010

MISHI B


Hatimaye ‘presenta’ wa kipindi cha miondoko ya Pwani kupitia Kituo cha Redio cha Magic FM cha jijini Dar es Salaam, Mwanahamisi Bashir Mwenda ‘Mishi B, hivi karibuni ameingia kwenye kitanzi cha ndoa baada ya kufanyiwa bonge la ‘kicheni pati’ ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuvaa pingu za maisha...
Shughuli hiyo iliyoshuhudiwa na Paparazi wa Mcharazo.blogspot.com, ilichukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Water Front Posta, jijini Dar juzi, ambapo mastaa lukuki walikuwa ndani.

Unaambiwa mbali na shughuli pevu ya mambo ya ndoa aliyobashiriwa na wafundaji maarufu, Mish B alijizolea zawadi na mapochopocho kibao ambapo haimuhitaji kufanya ‘shopingi’ kwa sasa isipokuwa ni kiasi tu cha kwenda kuanza maisha.

Katika hali ya maajabu, ndani ya ukumbi huo, huku Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Kopa akinogesha, ulifukizwa moshi mkali uliokuwa na harufu kali ya uturi kwa madai kwamba, kwa mwanamke yeyote aliyekuwa ndani ya ukumbi huo, ndoa yake haiwezi kuvunjika kirahisi baada ya kufukizwa moshi huo.

Hivi karibuni gazeti hili liliripoti habari ya Mishi B kuwa katika ‘prosesi’ za kufunga ndoa na mwanaume ambaye hakutajwa jina kwa sababu maalum.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Mishi B aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, mtangazaji huyo anatarajia kuolewa na mwanaume huyo baada ya kuwa katika uhusiano wa kawaida kwa muda mrefu.

Alisema kwamba, hatua ya Mishi B kuamua kubebwa jumla jumla imekuja kufuatia ushauri ambao watu wamekuwa wakimpa wakimweleza kuwa, kwa umri alionao sasa anastahili kuwa ‘Mrs’. Picha hizi ni kwa mjibu wa mtandao wa Zeze.

No comments:

Post a Comment