Saturday, March 20, 2010

WAKUSWAMPA KITAA

Pita pita yangu ilikuwa kimara,nini kilitokea huko?
Kaka mmoja mkazi wa kimara king’ongo wiki iliyopita yalimkuta maswaiba ya kutisha baada ya kumtongoza mwanamke mtaani hapo hapo anapoishi na kwenda kulala kwa dada huyo.Kaka huyo alistuka mishale ya saa nane usiku uso wake ulikutana na uso wa dada huyo ambaye ulikuwa wa mnyama aina ya punda.Dada huyo kuona soo hakamchimbia mkwara kaka huyo na kumwambia endapo hatatoa siri hiyo hatamfanyia kitu ambacho ajawai kufanyiwa tokea azaliwe,usiku huo huo kaka huyo alitimua mbio na kuondoka nyumbani hapo.Asubuhi ilipofika kaka huyo aliwatangazia watu wote wa kitongoji hicho kwa kuwaambia dada huyo ni mshirikina.Vijana waliamua kumpa jina la jini kabura,dada huyo mchana wa siku ya jumatano mishale ya saa nane alikodi pikipiki na kuondoka kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment